Ancelotti: Matokeo ya Ballon d'Or Yaheshimiwe

Kocha mkuu wa Real Madrid Carlo Ancelotti alikuwa na mkutano na wandishi wa habari siku ya Jumanne kuelekea mchezo wa Real Madrid dhidi ya Athletic Bilbao katika LaLiga.

Waandishi hawakuuliza maswali kuhusu mchezo huo pekee pia waligusia kuhusu tuzo za Ballon d’Or zilizofanyika siku ya Jumatatu.

Ushindi wa Leo Messi umezua mjadala mkubwa, lakini Ancelotti anahisi kwamba matokeo lazima yapewe heshima, ingawa alitamani mshindi wa Real Madrid katika toleo la mwaka ujao.

“Lazima uheshimu matokeo ya Ballon d’Or 2021. Messi ameshinda na bado ni mchezaji mzuri. Na hakuna cha kuongeza,” alisema.

“Kwa wachezaji, tuzo za mtu binafsi ni muhimu, lakini ikiwa hawatashinda, sio suala.

“Natumai mwaka ujao, mchezaji wa Real Madrid atashinda. Benzema alikuwa na msimu mzuri na alimaliza wa nne. Ataendelea na motisha ya kujaribu kuwa wa kwanza.”


MUDA WA KUJIACHIA NA CARNAVAL JACKPOT

Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe