Mchezo ulianza kwa timu zote zikishambulian kwa kushtukiza ambapo dakika 6 Yanga walikuwa wamepiga mashuti Mawili yaliyolenga goli.

Dakika ya 10 ya Mchezo KMC nao walipata kona ya Kwanza ambapo walishindwa kuitumia vizuri kupata bao la mapema, wakati huo Yanga wakionekana kulishambulia kwa kasi lango la KMC bila mafanikio.

Mshambuliaji Heritier Makambo alikosa nafasi nzuri ambapo alipiga shuti kulenga goli lakini litolewa nje na Yanga kuwafanya waongeze Idadi ya Kona kwa kufikisha kona 2 ndani ya dakika15 za kwanza.

Ilipofika Dakika ya 43, mashabiki wa Yanga walisimama na kupiga makofi kama ishara ya kumpongeza kocha wa timu hiyo Nasraddine Nabi kwa kufikisha mechi ya 43, bila kufungwa.

Yanga vs KMC, Yanga VS KMC Mechi ya Kibabe, Meridianbet

Dakika ya 44, KMC walikosa nafasi nyingine ya wazi kwa krosi iliyopigwa na Hance Msonga ambapo Matheo Antony akashindwa kumalizia, jambo ambalo liliiweka salama klabu ya Yanga, mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika ubao ulisomeka 0-0.

Kipindi cha Pili Nabi alifanya mabadiliko aliwaingiza wachezaji Moloko, Feisal na Mauya, kuchukua nafasi za Bakari Mwamnyeto, Dickson Ambundo na Tuisila Kisinda, ambapo mabadiliko hayo yalibadilisha mfumo wa uchezaji wa Yanga.

Na KMC walifanya mabadiliko mawili alitoka Awesu Awesu na Emmanuel Mvuyakule na kuingia Masoud Abdallah Darweshi Saliboko.

Dakika ya 35 ya mchezo Kiungo kutoka Zanzibar Feisal Salum aliwapatia bao la uongozi Yanga na kufanya ubao kusomeka 1-0.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa