Klabu ya Man Utd itapata wepesi wa kwenda hatua mtoano msimu huu ikiwa tu wataweza kuondoka na point kwenye mchezo wa Europa League siku ya Alhamisi dhidi ya Sheriff Tiraspol kwenye dimba la Old Trafford.

Ingawa Man Utd inashika nafasi ya pili kwenye kundi lao ambalo linaongozwa na Real Sociedad kwa pointi tatu, huku wote wakiwa wamecheza michezo sawa, pia Man Utd anafaida kwa sababu mchezo wa mwisho ambao unatarajiwa kuchezwa Novemba 3 utawakutanisha miamba hiyo.

Man Utd, Man Utd Matokeo Dhidi ya Sheriff Kuamua Hatma Yao Europa, Meridianbet

Ili klabu ya Man United isipate nafasi ya kucheza na timu ambazo zinatoka kwenye michuano ya ligi ya mabingwa inabidi ashinde mchezo wake wa kesho, na pia mchezo wake wa mwisho dhidi ya Real Sociedad.

Pia mchezaji nyota wa klabu hiyo Ronaldo amerudishwa kwenye kikosi cha timu hiyo, baada ya kuonesha utovu wa nidhamu kwenye mchezo dhidi ya Tottenham, na kuwekwa nje kwenye mchezo dhidi ya chelsea.

Anthony Martial na Raphael Varane wataendelea kukosekana, lakini Maguire, Donny van de Beek na Aaron Wan-Bissaka wameanza mazoezi na wapo kwenye uangalizi.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa