Klabu ya Barcelona imeaondolewa kwenye mashindano ya Ulaya hii leo baada ya klabu ya Inter Milan kushinda magoli 4 kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Giuseppe Meazza dhidi ya Viktoria Plzen.

Klabu ya Barcelona iko uwanjani ikicheza na klabu ya Bayern Munich ambapo mpaka dakika ya 45 akiwa anaongozwa kwa iadadi ya magoli mawili ambayo yamewekwa kimyani na Saidio Mane na Choupo-Moting huku kiongo wa zamani wa klabu ya Arsenal Gnabry ambaye  alitoa pasi hizo za magoli.

Barcelona

Ni timu mbili tu ambazo zitafuzu kwenda hatua ya kumi na sita kwenye kundi C ambazo ni Inter Milan na Bayern Munich huku Barcelona akienda kushiriki michuano ya Europa League.

Klabu ya Barcelon inatarajia kucheza na klabu ambayo itashika nafasi ya pili kwenye michuano ya Europa League ili kufanikiwa kucheza kwenye hatua ya mtoano.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa