Barcelona watamenyana na Bayern Munich saa leo jioni wakijua kwamba lazima washinde ili waweze kusalia na matumaini ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.

Bila shaka wakiwa Camp Nou, Xavi atachagua safu ile ile ambayo ilishinda Athletic Club 4-0 kutoka safu ya ulinzi, hadi ushambuliaji. Hiyo ina maana ya viungo wanne huku Pedri akicheza mbele kidogo.

Katika safu ya ulinzi, Alejandro Balde angeondolewa kwa Jordi Alba na Hector Bellerin angechukua nafasi ya Sergi Roberto aliyejeruhiwa. Xavi bado anawakosa Andreas Christensen, Ronald Araujo na Memphis Depay pia.

Kwa mujibu wa Diario AS inatabiri safu dhidi ya Bayern Munich inawakosa Manuel Neuer, Bouna Sarr, Lucas Hernandez na Leroy Sane.

Wachambuzi wa Sport na AS wanakubaliana juu ya safu ya Bayern pia, na Julian Nagelsmann alianzisha 4-2-3-1 akimshirikisha Eric Choupo-Moting kama mshambuliaji wao wa kati.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa