Ahmed Ally, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba amefichua ni kweli kuna mipango inafanyika kumhusu Cesar Lobi Manzoki raia wa DR Congo, lakini akaweka wazi kuwa mpaka sasa hakuna lolote kati yao na Bobosi Byaluhanga raia wa Uganda.

Manzoki na Bobosi wamekuwa kwenye rada za Simba tangu kipindi cha usajili wa dirisha kubwa ambapo kwa Manzoki, tayari walifikia makubaliano naye binafsi na kusaini mkataba wa awali wa miaka miwili kabla ya Vipers kuweka ngumu kwenye dau la usajili na straika huyo kutimkia China.

Ahmed Ally akubali usajili wa Manzoki

Dirisha dogo la usajili limefunguliwa rasmi leo Ijumaa ambapo linatarajiwa kuendelea kwa kipindi cha mwezi mmoja mpaka Januari 17, mwaka 2023.

Ally alisema: “Kumekuwa na taarifa nyingi kuhusu mipango yetu ya usajili na tayari baadhi ya wachezaji wamekuwa wakihusishwa moja kwa moja na Simba, wakiwemo Manzoki na Bobosi.

Ahmed Ally akubali usajili wa Manzoki

“Kuhusiana na Manzoki ni kweli nafahamu Uongozi umekuwa kwenye mipango ya kuhakikisha anakuwa mchezaji wa Simba, licha ya kuwa ni mapema kuzungumzia hili.

“Lakini Bobosi mpaka sasa nachojua hakuna mpango wowote wa kumsajili, labda kama kutakuwa na taarifa mpya kuhusu mahitaji ya kocha lakini kwa sasa niwaombe Wana Simba kuwa watulivu na kusubiri taarifa rasmi ya klabu.”

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa