Cesor Manzoki mchezaji wa klabu ya Vipers mabingwa wa ligi kuu ya uganda ameaga rasmi katika klabu hiyo.
Mchezaji huyo aliekua akihusishwa zaidi na wababe wa soka la Tanzania klabu ya Simba Sports zaidi ya miezi mitatu.
Mchezaji huyo raia wa Kongo amekua na wakati mzuri katika ligi kuu ya Uganda baada ya kua mfungaji bora wa ligi hiyo, tuzo ya anaeengoza kwa pasi za mwisho, pamoja na tuzo ya mchezaji bora wa ligi hiyo.
Simba wamekua wakitafuta mshambuliaji wa kiwango cha juu zaidi atakaeweza kuwasaidia kwenye michuano wanayoshiriki haswa micguano ya ligi ya mabingwa Afrika. Cesor manzoki baada ya kuaga klabuni kwake Vipers kumekua na maneno mengi juu ya uelekeo wa nyota huyo wengi wakiamini atajiunga na klabu ya Simba baada ya kuonekana kuvutiwa na klabu hiyo licha ya Vipers kuweka vikwazo juu ya kuondoka kwake lakini hatimae mchezaji huyo anaondoka klabuni hapo huku uelekeo wake ukiwa kitendawili.
Taarifa zingine zinaeleza anaelekea nchini China ambapo inaelezwa amepata klabu nchini humo mchezaji huyo keshaaga ndani ya klabu yake hiyon ya zamani masikio na macho ya wapenda soka yanasubiri kusikia na kuona ni wapi staa huyo atadondokea.