Anthony Santos kiungo mshambuliaji anayecheza kunako klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi aanadai anahitaji kuuzwa kwa gharama kubwa zaidi kwenye ligi hiyo uholanzi maarufu kama Eredivise.

Hii imekuja baada ya kuulizwa swali kwenye mahojiano aliyofanya na mwanahabari wa michezo nguli kutoka nchini Italia anayejulikana kama Fabrizio Romano ya kua kwanini klabu yake ya Ajax haitaki kumuachia aondoke na yeye kujibu kua yeye hajaomba Ajax imuachie bali yeye anahitaji kuuzwa kwa dau kubwa zaidi kwenye historia ya ligi hiyo.

anthony santos, Anthony Santos Anataka kuuzwa Gharama kubwa zaidi., Meridianbet

Anthony ameeleza zaidi kua kama klabu yake hiyo ikimuuza kwa dau hilo kubwa itawasaidia kujenga timu bila matatuzo yeyote ndo maana yeye alitaka auzwe kwa dau kubwa. Mshambuliaji huyo anashangazwa na klabu yake hiyo kukataa ofa kubwa ambayo imeletwa na klabu ya Man United mezani cha jumla ya kiasi euro milioni tisini.

Mchezaji huyo aliendelea kusisitiza kwenye mahujiano hayo msimamo wake upo palepale ni kuondoka ndani ya klabu hiyo na kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine kwani jambo hilo alikwishalifikisha kwa uongozi toka mwezi wa pili mwaka huu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa