Kiungo wa klabu ya Yanga Khalid Aucho amekumbana rungu la shirikisho la mpira la mpira wa miguu Tanzania (TFF) baada ya kumpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union Ibrahim Ajibu.

Khalid Aucho amelimwa faini ya shilingi laki tano za kitanzania pamoja na kukosa michezo mitatu ijayo katika ligi kuu ya NBC kutokana na kosa alilolifanya katika mchezo kati ya Coatal Union na Yanga.auchoKiungo huyo ambaye alikua anahusishwa na kufanya kitendo cha utovu wa nidhamu katika mchezo dhidi ya Ihefu ambapo klabu ya Yanga ilipoteza kwa mabao mawili kwa moja, Lakini mchezaji huyo hakupata adhabu.

Mbali na kiungo Khalid Aucho pia klabu yake imekumbana na adhabu ya kupigwa faini ya kiasi cha shilingi milioni tano kutokana na kitendo cha kuingilia mlango usioruhusiwa katika mchezo wa dabi dhidi ya Simba.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa