Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Uingereza Jude Bellingham amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora kijana inayofahamika kama Golden Boy.

Tuzo ya Golden Boy hutolewa kila mwaka kwa mchezaji kijana ambaye hajavuka miaka 25 na amefanya vizuri sana kwenye mwaka husika, Bellingham ametangazwa kubeba tuzo hiyo.bellinghamKiungo huyo raia wa kimataifa wa Uingereza ameanza vizuri sana kwenye klabu ya Real Madrid, Huku akifanikiwa kubeba tuzo za mchezaji bora wa mwezi mara kadhaa kwenye ligi kuu ya Hispania.

Kiungo huyo wa zamani wa Borussia Dortmund amefanikiwa kubeba tuzo ya mchezaji bora kijana wa mwaka katika usiku wa tuzo za Ballon Dor inayofahamika kama Kopa Trophy, Huku tuzo ya Golden Boy ndio ilikua ikisubiriwa na hatimae ametangazwa kama mshindi pia.bellinghamTuzo ya Golden Boy inatarajiwa kutolewa mwezi wa 12 tarehe nne katika jiji la Turin nchini Italia, Ambapo Jude Bellingham tayari ameshafahamika kama mshindi wa tuzo hiyo na hiyo ikitokana na muendelezo wa kiwango bora alichokionesha.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa