Katika mwendelezo wa Ligi kuu ya NBC hapo jana mechi ya saa moja usiku ni ile iliyowakutanisha Simba dhidi ya Dodoma Jiji, huku Jean Baleke ndiye aliyeisambaratisha timu hiyo kutoka Makao Makuu ya nchi.

Simba iliwakosa wachezaji wake muhimu takribani 9 kwenye mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo majeraha na adhabu za kadi za njano akiwemo Chama, Kanoute, Mzamiru na wengine.
Ndani ya dakika 45 za mchezo kabla ya kwenda mapumziko Jean Baleke ambaye ni usajili mpya wa Msimbazi aliingia kamabani na kuwapatia Simba bao la kuongoza ambao ndilo lililosalia mpaka mpira kumalizika.

Licha ya mpira kuwa mgumu, timu zote zilikuwa zinashambuliana huku Dodoma wakiwa wameahidiwa Milioni 30 endapo watawafunga Simba kitu ambacho kikafanya mpira kuwa na faulo nyingi kutokana na matumizi ya nguvu.
Hivyo Mnyama amefikisha pointi 50 baada ya ushindi wa jana na Dodoma wanafikisha mechi 6 bila kupata alama 3 kwa vijana wa Roberto baada ya kupanda ligi kuu Tanzania bara.

