Beki Azam Nje Miezi Mitatu

Beki wa kati wa klabu ya Azam FC Abdalah Kheri ‘Sebo’, atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti lake la mguu wa kulia.

Sebo ameumiza gegedu ‘cartilage’ ya maungio ya goti lake la mguu wa kulia, ambayo imelika na pia ameumiza mifupa midogo midogo kutokana na mlalo wa goti lake la kulia na tege alilokuwa nalo.azamBeki huyo kisiki, amefanyiwa upasuaji huo leo Jumatatu asubuhi, kwenye Hospitali ya Vincent Palloti, jijini Cape Town, Afrika Kusini.

Aidha, Sebo alipata majeraha hayo kwenye mchezo wa klab yake ya Azam dhidi ya Tanzania Prisons,

Daktari wa Azam FC, Dr. Mwanandi Mwankemwa, aliyeambatana na beki huyo, amesema kuwa Sebo atarejea kwenye soka la ushindani baada ya miezi mitatu ya matibabu ya majeraha yake kumalizika.

“Sebo amefanyiwa upasuaji wa kisasa unaoitwa arthroscopic, ambao wametoa mifupa midogo midogo iliyokuwa imevunjika na kupandikiza gegedu nyingine.azam“Baada ya kufanyiwa upasuaji huo, mchezaji ameelekezwa mazoezi ya kufanya kwa muda wa mwezi mzima na anatakiwa kupumzika kwa muda wa miezi mitatu,” alisema Dr. Mwankemwa

Acha ujumbe