Tuchel: Man United Presha ni Kubwa

Kocha wa klabu ya Bayern Munich Thomas Tuchel amesema kua tatizo kubwa linaloitafuna klabu ya Manchester United ni presha kubwa mabyo ipo kwenye klabu hiyo.

Kocha Tuchel anasema kua ndani ya Manchester United vitu vidogo vinageuka kua vikubwa tofauti na vilabu vikubwa akiona ni miongoni mwa mambo ambayo yanailetea shida klabu hiyo mara kwa mara.TuchelKocha huyo wa zamani wa Chelsea ameweka wazi kua jambo ambalo lingeonekana kua dogo sehemu nyingine basi ndani ya Manchester United jambo hilo linaonekana kua kubwa, Kwa maana hiyo hili ni jambo ambalo linawapa wakati mgumu kuanzia kocha mpaka wachezaji wake.

Kocha huyo pia alisema mambo makubwa ambayo aliyafanya kocha wa heshima aliyepita klabuni hapo Sir Alex Ferguson ni sababu pia inayochochea klabu hiyo kua kwenye wakati mgumu mara kwa mara.TuchelKocha Tuchel pia aligusia juu ya wakongwe wa klabu hiyo ambao mara nyingi huongea na kukosoa mambo kadhaa ndani ya klabu hiyo pia ni tatizo, Kocha huyo amezungumza hayo kuelekea mchezo wao wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Man United kesho.

Acha ujumbe