MENEJIMETI ya Klabu ya Yanga imesema kuwa wanajua kuwa kama watafanikiwa kuwafunga Al- Ahly kesho kutwa Jumamosi, itawapa fursa ya kupanda kwenye nafasi za juu kwenye ubora barani Afrika.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema, Rais wa Yanga Eng.Hersi Said anajua kuwa kuwafunga Al-Ahly ni alama ya ukubwa wao kwenye soka la Afrika na hiyo ndiyo sababu pekee ambyo inawafanya kufanya maandalizi makubwa kuelekea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Ali Kamwe alisema: “Tunakwenda kucheza na timu namba moja kwa ubora Afrika huo ndio ukweli lazima tujue hilo, na sisi tupo tano bora ya timu bora Afrika.
“Na ili uwe wa kwanza lazima umfunge yule namba moja na sisi Yanga SC tunaitaka ile namba moja yao. “Ndiyo maana wa Rais Yanga Eng. Hersi ameutolea macho kweli kwelu huu mchezo kwa sababu anajua kama tukiwafunga, Afrika nzima itajua kuwa Yanga sasa ni timu bora zaidi Tanzania na Afrika inauwasha moto.