Maguire Kugombea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi

Beki wa klabu ya Manchester United Harry Maguire amefanikiwa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha wachezaji sita watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa ligi kuu ya Uingereza.

Harry Maguire ameingia kwenye orodha ya wachezaji ambao watawania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Novemba kwenye ligi kuu ya Uingereza, Hiyo ikitokana na ubora aliouonesha hivi karibuni.maguireWachezaji wengine ambao wamechaguliwa sambamba na beki huyo ni Jeremy Doku wa Manchester City, Anthony Gordon wa Newcastle,Raheem Sterling wa Chelsea, Kamiski golikipa wa Luton Town, pamoja Marcus Tavernier wa klabu ya Afc Bournamouth.

Beki huyo wa kimataifa wa Uingereza miezi mitatu nyuma alikua kwenye kiwango cha chini sana mpaka klabu hiyo kufikiria kumuuza, Lakini siku za karibuni ameibuka shujaa ndani ya klabu hiyo kutokana na kiwango ambacho anakionesha katika michezo ya klabu hiyo.maguireUnaweza kusema majeraha muda mwingine ni baraka kwa wachezaji wengine, Kwani Maguire alipata nafasi baada ya mabeki wenzake Lisandro Martinez, Victor Lindelof, na Raphael Varane kupata majeraha kwa vipindi tofauti ndio beki huyo akapata nafasi.

Acha ujumbe