Onana Majanga Man United

Golikipa namba moja wa klabu ya Manchester United Andre Onana yuko kwenye kipindi kibaya ndani ya klabu hiyo kutokana na kiwango ambacho amekua akikionesha.

Andre Onana amekua kwenye kiwango kibovu ndani ya klabu hiyo haswa kwenye ligi ya mabingwa ulaya, Kwani amefanya makosa kadhaa kwenye michuano hiyo ambayo imepelekea klabu yake kuangasha alama.onanaGolikipa huyo mpaka sasa amefungwa mabao 14 kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ulaya, Lakini  magoli takribani matatu ni makosa ya moja kwa moja kutoka kwa golikipa huyo raia wa kimataifa wa Cameroon yakiwamo mabao mawili katika mchezo wa jana dhidi ya Galatasaray.

Mashabiki wa klabu ya Manchester United wamekua hawafurahishwi na kiwango cha golikipa huyo tangu kutua kwake klabuni hapo, Jambo ambalo limefanya hali ya kujiamini kwa golikipa huyo kushuka kwa kiwango kikubwa.onanaMbali na Onana kuonekana kua na kiwnago kibovu kwenye klabu hiyo lakini golikipa huyo anaongoza kwnye orodha ya magolikipa wenye hati safi kwenye michezo mingi ya ligi kuu ya Uingereza yaani kumaliza mchezo bila kuruhusu bao, Kwani kipa huyo hajaruhusu bao kwenye michezo mitano ya ligi kuu ya Uingereza mpaka sasa.

Acha ujumbe