KUELEKEA kwenye uchaguzi wa baadhi ya viongozi wa klabu ya Yanga ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibuni, aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya usajili na ufundi, Dominick Albinus ametoa ahadi ya kuboresha zaidi kikosi endapo atapata nafasi hiyo.
Albinus ni miongoni mwa viongozi wa Yanga ambao wamepeleka furaha ya mataji matatu katika klabu hiyo baada ya kufanya usajili wa baadhi ya nyota ambao wametimiza malengo hayo kwa msimu huu.
Bosi huyu, amenukuliwa akitoa ahadi yake kwa Wanayanga;
“Nimegombea nafasi hii kwa ajili ya kuhakikisha kuwa nikishirikiana na wenzangu tunaendeleza na kusimamia yale yote mazuri ambayo tuliyaanza na kuleta matunda.
“Naamini tukipata nafasi tutawaleta kina Mayele (Fiston) wengine ambao wataleta furaha zaidi Yanga kwa msimu ujao na lengo letu ni kuboresha zaidi kikosi chetu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa