Mshambuliaji mpya wa Simba Moses Phiri amesema kuwa anategemea kupata ushirikiano mzuri ndabi ya Simba kutoka kwa kiungo Clatous Chama na kuifanya Simba kuwa tishio zaidi kwa msimu ujao jambo ambalo anaamini litaisaidia timu hiyo kurejea katika makali yake.

Moses Phiri ndio usajili wa kwanza kutambulishwa ndani ya Simba kwa msimu huu ambapo mchezaji huyo ana uraia wa Zambia akama ambavyo ipo kwa Clatous Chama ambaye pia ni raia wa Zambia.

Phiri alisema kuwa anaamini kwa msimu ujao atapata usharikiano mzuri kutoka kwa Chama jambo ambalo litakuwa faida kwa Simba katika kuhakikisha kuwa wanairejesha Simba katika ubora wake.

“Nategemea kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa Chama kuelkea msimu ujao,Chama tumecheza wote katika timu ya taifa ya Zambia namfahamu vyema ni mchezaji mzuri sana na naamini kwa pamoja tutaipa ubora Simba kwa msimu ujao.”

“Simba msimu huu nafahamu haijakuwa katika ubora wake lakini naamini kwa msimu ujao kila kitu kitakuwa sawa,tuajitoa kwa uwezo wetu wote tushinde mataji,”alisema mchezaji huyo.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa