KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Angel Gamondi ameanza kuwapa jukumu mazito mchezaji mmoja mmoja ikiwemo Max Nzengeli, Pacome Zouzoua kuelekea mechi yao ya hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merrikh ya Sudan.

Hatua hiyo ni baada ya kocha huyo kuona ubora na madhaifu ya wapinzani wao kuhakikisha kila mchezaji wake anafanya majukumu yao ili kufanikisha ushindi katika mchezo huo wa Septemba 16, mwaka huu, nchini Kigali, Rwanda.GAMONDIKocha Gamondi alisema wiki hii ilikuwa ya mazoezi magumu kwa wachezaji wake na kuanza kutambua uwezo wa mchezaji mmoja mmoja kwa kiasi kikubwa.

Alisema ameona uwezo wa nyota wake akiwemo Max, Zouzoua na wengine wamefanya vizuri katika mechi zilizopita na hata mazoezi lakini anahitaji kuwa bora zaidi kuelekea mechi yao ijayo dhidi ya Al Merrikh.

“Kabla ya kwenda Rwanda, tutakuwa na mchezo mmoja wa kirafiki ambao tutatakiwa kucheza Jumamosi, naamini wachezaji wangu wanaendelea vizuri na tutafikia malengo yetu,” alisema kocha huyo.


Gamondi alisema ameuomba uongozi wa timu hiyo, kupata timu ya kucheza nayo kwa lengo la kuona maendeleo ya kikosi chake baada ya mazoezi makali.GAMONDIAliongeza kuwa, anaamini kwa asilimia 80 nyota wake wameimarika, anahitaji kikosi bora ambacho kitatoa ushindani katika kila mchezo.

 

Kikosi cha Yanga, wiki hii walikuwa na mazoezi ya nguvu baada ya kutoka ufukweni kwa wachezaji wakipata pumzi ya kutosha, Juzi na jana, nyota hao walifanya mazoezi ya ‘gym’ asubuhi na jioni uwanjani, lengo ni kuhakikisha timu inakuwa imara.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa