ROBERTINHO ALIA NA SAFU YA ULINZI

Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba Mbrazil Roberto Oliviera “Robertinho” ameibuka na kuitolea uvivu safu ya ulinzi ya timu yake,akieleza kutoridhishwa na ufanisi wao ambao unapelekea wapinzani kupata magoli.

Robertinho amesema hayo baada ya kuruhusu magoli mawili kwenye ligi na pia kuruhusu kwenye mechi za kirafiki walizocheza katika kipindi hiki ambacho ligi zimesimama.robertinho“Safu ya ulinzi bado haijakuwa sawa kwa asilimia 100,unaona jinsi gani tunapata bao lakini wapinzani wanaweza kurudisha, hii ni kutokuwa makini,nimewaeleza mabeki nini cha kufanya,”

“Nina imani kipindi hiki tutakitumia vyema kwa kuweka mambo sawa kwa programu ya mazoezi maalumu kwa mabeki ili kujiweka imara kabla ya kuelekea michuano ya kimataifa ambazo zinahusisha timu ambazo zinaijua vizuri Simba

Acha ujumbe