Gamondi Awatambia Azam Mapema

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema wanatambua mchezo dhidi ya Azam FC utakaopigwa wikiendi hii hautakuwa mwepesi licha ya kuwa na mwendo mzuri katika mechi zilizopita.

Kocha huyo amebainisha kwamba hawezi kusema kwamba watafunga mabao mengi kwenye mchezo huo kwa kuwa yeye hafanyi kazi ya ubashiri na anaheshimu Kila timu na uwezo wa Kila Mchezaji.gamondiMchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Jumapili ya Machi 17 saa 1:00 usiku ikiwa ni mzunguko wa pili,ikumbukwe kwamba mzunguko wa kwanza Yanga ilikomba pointi tatu mbele ya Azam FC.

Gamondi amesema:”Tumejiandaa vizuri kucheza na Azam FC tunafahamu kila mpinzani kuna namna yake ya kujiandaa kimbinu, Ukitazama matokeo yao ya hivi karibuni wameimarika hivyo lazima tuchukue tahadhari ya kutosha bila kujali matokeo yetu ya awali.

“Nina wachezaji wengi wazuri sana, tunaweza kucheza aina yoyote ya mchezo, iwe kushambulia, kumiliki mpira nk. Tunaweza kubadilika badilika kulingana na matakwa ya mchezo kabla na wakati wa mchezo, sijawahi kucheza na aina moja ya falsafa huwa nabadilika kulingana na namna mpinzani anavyocheza na namna navyoweza kumkabili.gamondi“Mechi nne tumefunga magoli 16, tumeruhusu bao 3, kimsingi hizi ni takwimu bora siwezi kusema kwamba Azam nao tutawafunga magoli mengi huo utakuwa ubashiri sifanyi kazi ya kubashiri, ninachoweza kufanya kwa sasa ni kujiandaa kushinda mchezo huo.

“Tumejiandaa kucheza nao kwa namna yoyote ambayo watajipanga, nafikiri watakuja na mbinu za kushambulia lakini hainipi hofu kwa sababu nina vijana wazuri,”Alisema Gamondi

Acha ujumbe