Yanga SC imepanga kumuongezea mkataba wa miaka miwili kocha raia wa Argentina Miguel Gamondi utakaomalizika mwaka 2026.
Yanga wamefikia hatua hiyo baada ya kuridhishwa na ubora wa Kocha huyo, huku mipango ikiwa ni kuwa na mwalimu ambaye ameshazijua njia za ushindi.
Ali Kamwe ameiambia Meridian Sports kuwa, mpango huo umeshakamilika na Gamondi ataongeza mkataba mpya muda mfupi Baada ya kurejea kutoka mapumzikoni.
“Gamondi mkataba wake ulikua unaisha kabla ya msimu kuanza na uongozi umeona ipo sababu ya kumpa mkataba mpya.