Benchi la ufundi la timu ya Ihefu limefunguka kuwa hali ambayo wanapitia kwa sasa ni ya kawaida kama ambavyo wengine waliwahi kupitia.

Leo jumamosi saa 1:00 usiku kikosi cha Ihefu kitashuka dimba la Mkapa kumenyana na Simba ukiwa ni mchezo wa ligi kuu.

Akizungumzia maandalizi yao kuelekea kwenye mchezo wa leo dhidi ya Simba, Kocha Msaidizi wa Ihefu, Temmy Felix alisema maandalizi yamefanyika kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya mchezo huo.

“Maandalizi yetu yamekamilika kwa asilimia kubwa kuelekea kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Simba na tunatambua kuwa utakuwa ni mchezo mgumu.

“Ni kweli tunapitia katika kipindi kigumu lakini kila mmoja amewahi kupitia hivyo ni kawaida kwenye soka.

“Hivi karibuni tumekuwa tukipambana kupata matokeo na nafasi nyingi zinatengenezwa hivyo katika mchezo huu tutaenda kupambana.”

aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa