Simba Queens watacheza mechi ya kutafuta mshindi wa tatu leo dhidi ya Bayelsa Queens katika michuano ya Klabu bingwa barani Afrika kwa upande wa wanawake.

Mchezo huo utapigwa saa 4:00 usiku nchini Morocco kwa ajili ya kutafuta mshindi wa nafasi ya tatu katika hayo mashindano.

Kocha Mkuu wa Simba Queens, Charles Lukula alisema kuwa “Maandalizi yamekamilika na tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo.

“Wachezaji wana morali ya kuhakikisha matokeo yanapatikana kwenye mchezo wa leo kwa ajili ya kuhakikisha tunakuwa washindi wa nafasi ya tatu kwenye mashindano.

“Ni kweli tulipoteza mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Mamelod Sundown lakini kwa sasa nimewaeleza wachezaji kwamba ni lazima turudi na medali nyumbani.”

aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa