Taarifa njema kwa mashabiki wa Simba ni juu ya kitasa cha klabu hiyo raia wa kimataifa wa Congo Henock Inonga ambaye kwa mujibu wa taarifa kutoka Hospitali ya Temeke hajapata majeraha makubwa sana.
Inonga ambaye alitolewa nje na machela katika mchezo dhidi ya Coastal Union leo baada ya kuchezewa rafu mbaya na mchezaji Haji Ugando, Taarifa zinasema amepata mchubuko kwenye ugoko na anaendelea vizuri anaweza kuruhusiwa mda wowote.
Kutokana na rafu ambayo alichezewa beki huyo wengi waliamini huenda amepata jeraha kubwa ambalo lingemueka nje ya uwanja kwa muda mrefu, Lakini sio hali halisi kwani taarifa zimeweka wazi beki huyo hajapata majeraha makubwa.
Taarifa hiyo imekua kama baraka kwa mashabiki wa Simba ambao walionekana kukosa raha licha ya ushindi ambao wameupata dhidi ya Coastal Union, Kwani beki huyo amekua roho ya safu ya ulinzi ya klabu hiyo kwa msimu wa tatu sasa.
Beki Inonga Baka amekua akiandamwa na majeraha mara kwa mara sasa kwani ametoka kuuguza majeraha ya mkono siku kadhaa nyuma, Huku leo akipata jeraha lingine ambalo lilikadiriwa kubwa japo sio jeraha kubwa kama ilivyobainishwa.

