Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ambaye anakipiga katika klabu ya Inter Miami ya nchini Marekani kwasasa amesema hafikirii kuhusu kombe la dunia lijalo mwaka 2026 kwasasa.
Messi amesema kwasasa anawaza michuano ya Copa America ambayo itapigwa mwaka 2024, Lakini suala la kombe la dunia mwaka 2026 staa huyo haoni kama ni kipaumbele chake kwasasa.
Staa huyo amekua kwenye kiwango bora sana kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar na kuiwezesha timu ya taifa ya Argentina kuweza kubeba kombe lake la dunia tatu katika historia ya nchi hiyo.
Nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Barcelona na PSG anasema ni miaka mingi imepita sasa na ataangalia siku baada ya siku kwa namna ambavyo maendeleo yake ya mwili yatakua lakini kwasasa anafikiri zaidi kuhusu michuano ya Copa America.
Ikiwa ni chaguo la mashabiki wa timu ya taifa ya Argentina bado wangependa Messi aendelee kukipiga katika timu hiyo kutokana na mambo makubwa ambayo ameyafanya katika timu hiyo katika kipindi chote ambacho ameitumikia timu hiyo.


