Kibu Denis Kuiwahi Mtibwa Sugar

Mshambuliaji wa klabu ya Simba Kibu Denis inaripotiwa kua atakuwepo katika mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya klabu ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kupigwa kesho mkoani Morogoro.

Mshambuliaji Kibu Denis ambaye alipata majeraha ya goti na kudhaniwa huenda akaukosa mchezo huo ambao utapigwa kesho Jumamosi, Lakini taarifa zinaeleza mchezaji huyo atakuepo katika mchezo huo kwajili ya kuhakikisha Mnyama anapata alama tatu muhimu katika mchezo huo.kibu denisKocha wa klabu ya Simba Robertinho amesema kua mchezaji huyo ni moja ya wachezaji wanaojituma kikosini, Pia akieleza mchezaji huyo aliumia kidogo lakini kwasasa amekua akifanya mazoezi na timu hivo ni wazi atakuepo katika mchezo huo wa ligi kuu ya NBC.

Kibu Denis amekua moja ya mchezaji ambaye kocha wa klabu ya Simba anawahusudu sana na kumuona kama mchezaji muhimu zaidi kwenye timu hiyo, Hivo taarifa za kurejea kwa mshambuliaji huyo inaaminika ni habari ambazo zimemfurahisha kocha huyo.kibu denisKlabu ya Simba kesho itashuka dimbani dhidi ya klabu ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya NBC, Hivo kurejea kwa Kibu Denis kutoka katika majeraha yake ya goti kutaongeza nguvu kwenye kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kuelekea mchezo huo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.