Klabu ya KMC imetamba ndani ya mwezi Septemba na hiyo ni baada ya kutwaa tuzo mbili katika ligi kuu ya NBC baada ya kubeba tuzo ya kocha bora wa mwezi na tuzo ya mchezaji bora wa mwezi.
KMC imetoa kocha bora wa mwezi wa ligi kuu ya NBC ambaye ni Abdihamid Moalin na mchezaji bora wa mwezi akichukua Waziri Junior ni baada ya kuonesha ubora mkubwa katika michezo miwili ya mwezi Septemba.
Klabu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni ilifanikiwa kukusanya alama sita katika ligi kuu ya NBC kwenye michezo miwili ambayo waliicheza kwenye mwezi huo, Ambapo ndio sababu iliyosababisha wabebe tuzo hizo.
Kocha Moalin amefanikiwa kubeba tuzo hiyo akiwashinda makocha wawili ambao ni kocha wa Simba Robert Oliviera Robertinho na kocha wa Mashujaa Abdallah Mohamed na hiyo ni kutokana na kuiongoza klabu hiyo kushinda michezo yake miwili.
Mchezaji Wazir Junior yeye amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi baada ya kufunga mabao mawili katika michezo miwili aliyocheza na kuiongoza klabu yake ya KMC kuchukua alama sita, Lakini pia alifanikiwa kuwapiga chini wapinzani wake ambao walikua ni Jean Baleke wa Simba, na John Nakibinge wa Tabora United.

