Klabu ya Simba imefanikiwa kushinda mchezo wake wa ligi kuu ya NBC dhidi ya klabu ya Tanzania Prisons uliopigwa katika dimba la Sokoine jijini Mbeya ambapo wameitandika timu hiyo kwa mabao matatu kwa moja.
Simba wamefanikiwa kuchukua alama tatu muhimu mbele ya Prisons katika mchezo mgumu na kuwafanya wekundu wa Msimbazi kushinda michezo yao yote minne ambayo wameicheza mpaka sasa.Wekundu wa Msimbazi walianza kwa kasi ya chini katika dakika 15 za kwanza jambo ambalo liliwafanya Prisons kupata bao la mapema kupitia kwa Edwin Balua, Ambapo Mnyama alifanikiwa kutulia na kusawazisha bao dakika ya 34 Clatous Chama kabla ya John Bocco kuweka bao la pili.
Mchezo huo ulienda mapumziko kwa Mnyama kua mbele kwa mabao mawili kwa moja kupitia mabao ya John Bocco na Clatous Chama,Kipindi cha pili kikionekana kua kigumu zaidi ambapo Prisons walionekana kutafuta bao la kusawazisha na matumizi ya nguvu zaidi.Klabu ya Simba sasa wapo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya kushinda michezo yote minne na kufikisha alama 12, Huku wapinzani wao klabu ya Yanga wakiwa na alama 9 wakishika nafasi ya tatu nafasi ya pili wakishika klabu ya Azam wakiwa na alama 10.