Kaimu kocha Mkuu wa kikosi cha Coastal Union, Joseph Lazaro ametoa lawama kwa uongozi juu ya kumuondoa aliyekuwa Kocha Mkuu, Yusuf Chippo.

Coastal Union jana jumanne ilicheza mchezo wa ligi dhidi ya Yanga ambao walipoteza kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Kocha Coastal afunguka mazito

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Lazaro alisema “Leo tumefungwa kwa uwezo mkubwa walionao wachezaji wa Yanga.

Kocha Coastal afunguka mazito

“Wachezaji wa Yanga kocha wao hafundishi bali anaingiza mfumo sisi makocha wa timu zingine tunafundisha kuanzia mazoezini mpaka kwenye mechi hilo ni tatizo”.

“Kingine kilichofanya tufungwe leo ni kuondoka kwa kocha Chippo huwezi kumfukuza kocha leo na kesho kuna mechi, tunavunja morali ya wachezaji na viongozi wanapaswa kuwa wavumilivu wakati mwingine.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa