ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Namungo, Mzambia, Honour Janza ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya Zesco United ya Zambia ikiwa ni muda mfupi tangu aondoke nchini.
Janza ameteuliwa katika nafasi hiyo ambapo kwa sasa atakuwa ni bosi wa aliyekuwa kocha wa zamani wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina.
Taarifa za uhakika kutoka chini Zambia zinaeleza kuwa, Janza amekula shavu hilo ikiwa ni muda mchache tangu ajiuzulu kuinoa Namungo ambayo imemteua kocha wa zamani wa Simba, Denis Kitambi kurithi nafasi yake.
“Ni kweli, Janza ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Zesco, na hii imekuwa muda mfupi tangu aliapoachana na Namungo ambapo kwa sasa atakuwa yeye ndiyo bosi wa Lwandamina ambaye amerejea siku chache zilizopita ndani ya Zesco.”
Kwa mujibu wa taarifa mbayo imetolewa kwenye na uongozi wa timu hiyo, umethibitisha kumteua kocha huyo wa zamani wa Namungo na Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars kuteuliwa katika nafasi hiyo.