Refa Aliyechezesha Mechi ya Argentina vs Uholanzi Afungiwa

Lionel Messi anapata matakwa yake! Refa asiyependwa na watu wengi Mateu Lahoz ‘arudishwa NYUMBANI kutoka kwenye Kombe la Dunia ikiwa ushindi wa Argentina dhidi ya Uholanzi ndiyo mchezo wake wa mwisho nchini Qatar’ – huku mwamuzi huyo wa Hispania akitoa kadi 15 za njano katika mchezo mkali wa robo fainali.

 

Argentina

Mateu Lahoz hatachezesha mechi yoyote kati zilizosalia kwenye Kombe la Dunia huku ‘akirejea nyumbani kutoka Qatar’, kwa mujibu wa COPE.

Mchezo wa mwisho wa mwamuzi ulikuwa mpambano mkali wa robo fainali kati ya Argentina na Holland ambapo alitoa kadi 15 za njano.

Utendaji wa Lahoz haukupokelewa vyema na timu zote mbili – huku wachezaji wa Argentina wakizungumza hasa kuhusu maamuzi yake.

Nahodha na nyota wa Argentina, Lionel Messi, aliongoza shutuma za Lahoz kufuatia mchezo huo.

 

Argentina

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 aliendelea: “Nafikiri Fifa lazima ishughulikie hili, haiwezi kumweka mwamuzi kama huyo kwenye mechi ya ukubwa kama huo, yenye umuhimu mkubwa. Mwamuzi hawezi kushindwa kuwajibika.”

Inaweza kuonekana kuwa Messi amekubaliwa matakwa yake na Fifa – kutomruhusu kuwa mwamuzi katika nusu fainali au fainali.

Kipa wa Argentina Emi Martinez aliungana na nahodha wake kukosoa maamuzi ya mwamuzi huyo.

 

Argentina

Martinez alisema: “Mwamuzi alikuwa akitoa kila kitu kwa ajili yao.

“Alitoa dakika 10 [muda ulioongezwa] bila sababu. Alikuwa akitoa adhabu za faulo nje ya eneo la hatari kwa ajili yao, kama mbili, mara tatu. Alitaka wafunge tu, ndio hivyo. Kwa hivyo, tunatumai hatutakua na refa huyo tena. Yeye hana maana.”

Licha ya kumkosoa mwamuzi, tofauti na Lahoz, kampeni ya Argentina Kombe la Dunia inaendelea.

Messi na wenzake, wanamenyana na Croatia katika nusu-fainali huku wakipania kujikatia tiketi ya kucheza fainali ya Kombe la Dunia.

Beti mechi zijazo za kombe la dunia na nyingine kupitia Meridianbet, beti na kitochi bila bando, kwenye machaguo spesho ya kombe la dunia yenye ODDS kubwa na bomba, na kama sio mpenzi wa mpira kuna michezo ya kasino mtandaoni napo unaweza kushinda jakipoti kubwa. Beti hapa.

Acha ujumbe