Nahodha msaidizi wa timu ya taifa ya Pepe Lima ametupia lawama mamlaka zinazohusika na uandaaji wa michuano ya kombe la dunia kwa kulaumu haikubaliki wachezeshwe na refa kutokea Argentina baada ya kutolewa na Morocco leo.

Ureno imetupwa nje ya michuano ya kombe la dunia katika hatua ya robo fainali na timu ya taifa ya Morocco kwa bao moja kwa bila. Na ndipo mkongwe huyo akaibuka baada ya mchezo na kudai kua kilichotokea hawajakubaliana nacho hata kidogo.pepe“Haikubaliki kwa refa wa Kiargentina kuchezesha mchezo wetu, Nimehuzunika sana. Zilikua dakika 90 ambazo alitaka kusimamisha mchezo wetu kwa faulo ndogondogo na refa hakutoa kadi yeyote” Alisema Pepe Lima

Mkongwe huyo pia alienda mbali kwa kuona kua kama michuano hiyo imeandaliwa ili Argentina wawe mabingwa kwani ameeleza kuna vitendo alifanya Messi jana ambavyo si vya kiungwana lakini hakuna hatua yeyote ilichukuliwa na kusema wazi wawape Argentina tu kombe hilo.pepeFacundo Tello Muargentina ambaye alisimamia mchezo kati ya Ureno dhidi ya Morocco ikishuhudiwa Morocco wakiandika historia kwa taifa lao na bara la Afrika kwa ujumla amepata lawama kutoka kwa Pepe akidai alikua na lengo la kuhakikisha wanatoka kwenye michuano hiyo.

 JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa