Simba Yafanya Kufuru kwa Mkapa

Klabu ya soka ya Simba imeanza kampeni yake ya michuano ya Shirikisho ya Azam kwa staili ya aina yake baada ya kuibuka na ushindi mnono wa magoli nane kwa bila dhidi ya klabu ya Eagle Fc.

Klabu ya Simba imefanikiw kutoa adhabu hiyo kali katika mchezo uliopigwa katika dimba Benjamin Mkapa jijini Dar-es-salam ambapo wekundu wa Msimbazi walitandaza soka safi na kuweza kupata ushindi mnono kabisa katika mchezo huo.simbaMabao nane ya klabu ya Simba yaliwekwa kimiani na Moses Phiri Jenerali alieweka kambani mabao manne, Habib Kyombo akifunga bao moja Clatous Chama Mwamba wa Lusaka akiweka mabao mawili na Pape Osmane Sakho akifanikiwa kufunga bao na kukamilisha karamu ya mabao kwa mnyama.

Mnyama anaendeleza rekodi yake ya kua timu inayoongoza kwa kufunga mabao mengi baada ya kufanya hivo kwenye ligi kuu ya NBC na sasa wamehamishia kwenye kombe la shirikisho la Azam, Kwakua mpaka sasa ndio wanaongoza kwakua timu iliyofunga mabao mengi kwenye ligi hiyo.

Acha ujumbe