Kuhusu Manula Kwenda Azam FC, Ahmed Ally Afafanua.

AFISA HABARI wa Simba SC Ahmed Ally ameweka wazi hatma ya mlinda mlango wao mzawa Aishi Manula ambaye anahusishwa zaidi na kujiunga na wanalamba lamba wa Chamazi Azam FC. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Klabu ya Azam FC inaelezwa kwamba imeiandikia barua Uongozi wa Simba kuhitaji huduma ya mlinda mlango wao Aishi Manula.

Lakini hadi sasa Uongozi wa klabu hiyo bado hawajaijibu barua hiyo, kwa taarifa zilizopo kutoka ndani ya klabu ya Simba ni kwamba Aishi Manula yupo kwenye mahesabu ya kumtoa kwa mkopo kipa huyo, au kumuuza moja kwa moja.

Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.

Alipohojiwa na Azam Media Ahmed Ally alisema kwamba msimu ujao watakuwa na makipa wao akiwataja kwa majina, Lakred, Ally Salim na Hussein Abel lakini jina la Aishi Manula hakulitaja.

“Bila shaka unamzungumzia Aishi Manula, ni taarifa hata mimi binafsi nimeziona mitandaoni ila sijapewa taarifa kutoka kwa Viongozi wangu, bado ana mkataba wa mwaka mmoja siwezi kusema kama ntutaomtoa kwa mkopo au tutamuuza, lakini nithibitishe kwamba Ayub Lakred tunae, Ally Salim tunae na Hussein Abel yupo.

Soka La Bongo tuliripoti juu ya taarifa za kuhitajika kwa Aishi Manula na klabu ya Azam FC, lakini hadi sasa Uongozi wa timu hiyo umekuwa ukificha sana taarifa za mlinda mlango huyo.

Azam FC wanataka kuimarisha timu yao kuelekea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, hivyo wanahtaji wachezaji wakubwa na wazoefu na wanaamini uzoefu na ukomavu wa kipa huyo namba moja wa Taifa Stars utaenda kuwasaidia sana kwenye timu kufikia malengo yao.

Kasino ya Mtandaoni usipange kuacha kucheza, Meridianbet wameakuandalia Maokoto na bonasi za kasino kibao.

Acha ujumbe