Raya Asaini Mkataba wa kudumu Arsenal

Golikipa wa klabu ya Brentford David Raya ambaye alikipiga kwa mkopo klabu ya Arsenal  msimu uliomalizika amefanikiwa kusaini mkataba wa kudumu ndani ya klabu ya Arsenal.

Golikipa wa kimataifa wa Hispania David Raya amekua na msimu mzuri ndani ya klabu ya Arsenal msimu uliomalizika jambo ambalo limewafanya washika mitutu hao kutoka jiji la London kuamua kumpa mkataba wa kudumu ambao utaendelea kumuweka ndani ya klabu hiyo muda mrefu zaidi.rayaPaundi milioni 27 ndio kiasi ambacho kilikua kwenye mkataba wa golikipa huyo ndani ya klabu ya Brentford ambapo klabu itakayoweza kulipa kaisi hicho itampata mchezaji huyo, Klabu ya Arsenal wamefanikiwa kulipa kiasi hicho na kufanikiwa kumpata golikipa huyo wa kimataifa wa Hispania.

Kocha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta ameweka wazi sababu zilizofanya wakampa mkataba wa kudumu mchezaji huyo ndani ya klabu “David Raya alituonyesha msimu uliopita jinsi alivyo mchezaji muhimu kwetu, kwa hivyo tunafurahi sana kwamba sasa rasmi ni mchezaji wetu.”

“Ana mchango mkubwa katika chumba chetu cha kubadilishia nguo na tunafurahi sana kuendelea kufanya kazi naye”.

Acha ujumbe