Kocha Simba Afunguka Makubwa, Amtaja Manula na Robertinho

KOCHA wa Makipa wa Simba Dani Cadena ametoa ushauri kwa Viongozi wa klabu hiyo. kwamba ili timu hiyo ibadilike inapaswa kuajiri watu wenye uzoefu, bila kuangalia majina yao, na leseni pekee. Jisajili na Meridianbet upate bonasi za kasino kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.

Cadena ambaye hivi karibuni alionekana kuanza utaratibu wa kuwaaga mashabiki kwenye mechi za mwishoni, akiwapatia vifaa vyake, inaelezwa kwamba hana mpango wa kuendelea kusalia Simba endapo hakutafanyika mabadiliko.

Dani Cadena alisema kwamba; “Viongozi waondoe watu wengi sio mimi tu bali kila mtu asiyekuwa na uwezo, Simba inahitaji watu wenye taaluma, uwezo mkubwa na uzoefu, sio tu kwa watu wenye majina makubwa, leseni au katoka eneo gani sio hivyo”

Hata hivyo pia kcha huyo wa Makipa alielezea jinsi ambavyo alikataza golikipa wa klabu hiyo Aishi Manula asicheze mchezo wa dabi, kwa sababu alikuwa hajapona vizuri, lakini kocha Mkuu wa kipindi hicho Robertinho akamtaka acheze hiyo mechi, ambayo Simba iliambulia kipigo cha aibu kutoka kwa watani zao 1-5. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

“Siku mbili kabla ya mechi, katika kikao na viongozi wa bodi hakuna hata mmoja aliyeniuliza kuhusu hali ya utimamu wa mwili wa Aishi Manula, lakini Robertinho alisema Aishi Manula yuko fiti atacheza”

“Baadae nilienda kuongea na Manula nikamwambia mechi ya Kesho kama unataka kucheza utacheza, lakini najua haupo fiti, mimi ni kocha najua wachezaji wangu, lakini sikushauri acheze kwa sababu nilijua kitakachotokea, na kweli baada ya mechi tulipoteza kwa 1-5.

Ifahamike kwamba Mkataba wa Dani Cadena Simba unamalizika Juni 30, na hana mipango ya kuongeza mkataba mwingine hadi pale mabadiliko yatakapofanyika ndani ya klabu hiyo.

Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.

Acha ujumbe