Ubaya Ubwela ya Simba Imekubali, Mikumi Kumenonga.

UBAYA UBWELA, Mashabiki wa Simba SC wameitikia wito katika safari ya kwenda Hifadhi ya Mikumi mkoani Morogoro kwa ajili ya uzinduzi wa Simba Day ambapo kilele kitakuwa Agosti 3 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Katika kutambua umuhimu wa kutangaza vivutio vya utalii nchini, Simba iliamua kufanya uchaguzi wa kuzindua wiki ya kuelekea tukio hilo katika Hifadhi ya Mikumi ambayo Agosti 7, mwaka huu ilifikisha miaka 60 tangu kuanzishwa. Ubaya Ubwela Imekubali.

Kama ambavyo ilitangazwa na viongozi wa Wekundu wa Msimbazi, mashabiki ilibidi waripoti saa 11:00 alfajiri leo katika Stesheni ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) iliyopo Posta jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza safari saa 12:00 asubuhi kwa treni ya umeme maarufu SGR.

Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi  zinakaribia kuanza,  usije kupishana na gari la Mshahara.

Licha ya muda huo wa kuripoti wapo ambao walifika mapema zaidi na wengine ilidaiwa walikesha hapo ili kupata nafasi ya kuwa sehemu ya tukio hilo ambalo lilielezwa kuwa ni bure kwa mabehewa matatu.

Ndani ya muda mfupi kulingana na idadi kubwa ya mashabiki waliojitikeza mabehewa hayo yalijaa mapema huku mashabiki wengine ikiwalazimu kukata tiketi kwa fedha zao kweli Simba ya Ubaya Ubwela Iko moto.

Uzinduzi huo ni kuelekea kwenye kilele cha tamasha la 16 la Simba Day ambapo huanza kwa wiki nzima wanachama na mashabiki wa timu hiyo katika matawi yote nchini kufanya kazi za kujitolea kwa jamii na kutoa misaada mbalimbali kwa wenye uhitaji.

Katika siku ya kilele mashabiki na wanachama hukusanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa tangu asubuhi ambako huwa na burudani mbalimbali zinazoongozwa na wasanii, muziki, ngoma na michezo mbalimbali ikiwamo kutambulishwa kwa kikosi kipya kabla ya kuhitimisha kuingia uwanjani kucheza mechi na mwaka huu itakipiga dhidi ya APR ya Rwanda.

Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.

Acha ujumbe