TAMASHA la Simba Day ambalo limefanyika leo jumatatu kwenye Uwanja wa Benjamini Wiliam Mkapa maarufu kama Lupaso limesheheni mambo mengi na moja ya sapraizi ni kuwepo kwa bondia Shaban Kaoneka.

Kaoneka ambaye alipigana na Mandonga Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma hivi karibuni na kuibuka na ushindi raundi ya nne ya pambano hilo.

Kaoneka, Kaoneka Ndani ya Simba Day, Meridianbet

Kaoneka alionekana uwanjani hapo hiyo ikiwa ni siku moja baada ya bondia aliyepigana naye, Karim Mandonga kuhudhuria tamasha la kilele cha siku ya mwananchi kilichofanyika jumamosi.

Katika tamasha la Simba Day limeweka rekodi mojawapo ikiwa ni kuujaza uwanja wa Mkapa mapema huku pia wasanii mbalimbali wakitumbuiza akiwemo Zuhura Othman ‘Zuchu’.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa