BAADA ya kumaliza kambi ya nchini Misri, kikosi cha Azam FC kimerejea nchini leo tayari kwa ajili ya maandalizi ya tamasha lao la AZAMKA litakalofanyika Agosti 14, mwaka huu.

Tamasha hilo litafanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar ambalo litakuwa maalum kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wao.

Katika siku hiyo pia utapigwa mchezo wa kirafiki kati ya Azam dhidi ya Zesco United kutoka Zambia.


Baada ya kukamilika kwa kambi yao, Kocha Mkuu wa Azam FC, Abdihamid Moallin amesema kuwa “Kwa ujumla kazi kubwa imefanyika uzito mzuri wa mazoezi kujitoa kwa hali ya juu kwa wachezaji.

“Umekuwa mchakato mzuri kwetu kufanya haya maandalizi na kwa upande wetu tumefurahishwa sana na kazi tuliyoifanikisha kwa muda wote.”


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa