Ihefu Yatumia Mbeya Super Cup Kujiandaa na Ruvu

Kocha Mkuu wa Ihefu Zuber Katwila amefunguka kuwa mashindano yao ya Mbeya Kwanza Super Cup wanayatumia kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting.

Kwenye mashindano hayo ya Mbeya Super Cup ambayo yanafanyika mkoani Mbeya tayari Ihefu wamecheza mechi moja dhidi ya Mbeya City na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

 

Akizungumzia hilo Katwila amesema “Tunamshukuru Mungu kikosi kipo salama kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi.

“Kesho tunatarajia kucheza mechi ya pili ya mashindano ya Mbeya Super Cup na haya mashindano tunayatumia kwa ajili ya maandalizi ya michezo yetu ya ligi.

“Kikosi kwa sasa kinaonekana kuwa na muunganiko kwani hata wachezaji ambao tumewasajili wana uzoefu hivyo tuna imani watatusaidia.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.