Tajiri MO Dewji Hataki Masihara, Aanza na Usajili, Mambo 6 Kipaumbele Zaidi

MO Dewji: Juni 11, 2024 itabaki kumbukumbu kwenye vitabu vya soka haswa kwa mashabiki na wanachama wa Simba, ambapo Salim Abdallah Try Again alitangaza rasmi kujiuzulu Uenyekiti wa Bodi   ya Wakurugenzi, kufuatia changamoto zilizoikumba klabu hiyo ikianguka kwa matokeo kwa kushika nafasi ya tatu kwenye msimu uliomalizika. Jisajili Meridianbet kufurahia ubashiri  wa mechi nyingi, Simba mpya inakuja.

Akitangaza muda mfupi uliopita MO DEWJI ameridhia kurejea kwenye kuongoza bodi ya klabu hiyo kuhakikisha anarejesha utulivu ambao ulipotea ndani ya miaka mitatu.

Katika taarifa yake kwa Wanasimba MO DEWJI ameyataja mambo sita yaliyoikwamisha Simba yakiwemo mvurugano na makundi yaliyozalishwa na uchaguzi wa viongozi wa juu kwa upande wa wanachama.

“Tangu uchaguzi upite tumekuwa na mvurugano na makundi yaliyotokana na uchaguzi, hili limesababisha migongano mbalimbali ndani ya klabu yetu, niwaombe Wanasimba wenzangu tuvunje makundi na turudi kushirikiana kama kauli yetu inayosema Simba Nguvu Moja,”amesema MO.

Ameelezea pia namna mabadiliko ya benchi la ufundi na eneo hilo kutokuwa imara limechangia kuirudisha nyuma timu hiyo kongwe. Simba imara inarudi, usiwaze kuchana mkeka wako, jiandae kwa ushindi kutoka Meridianbet, Bashiri michezo  mingi.

“Tulipoteza ubora wa kucheza mpira wetu wa ‘pira biriani’ kutokana na mabadiliko ya makocha, nitashirikiana na viongozi wenzangu kuunda benchi imara la ufundi litakaloturudishia ubora wetu.”

Tajiri huyo ameutaja pia usajili usiokidhi kiu ya Wanasimba ukichangia kuirudisha nyuma timu hiyo kutawala kwa kuchukua vikombe vya ndani ya nchi.

“Tumekuwa tukisajili wachezaji wengi ambao wameshindwa kukidhi kiu ya Wanasimba, nataka niwaambie Wanasimba tutakwenda kufanya usajili mzuri utakaorudisha ubora wa kikosi chetu.”

Ameelezea pia kutokukamilika kwa mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji na kwamba wanakwenda kuhakikisha hatua zilizosalia zinamalizika sambamba na kuboresha miundo mbinu ya viwanja vyao ya mazoezi vilivyopo Bunju ambapo amekiri kuwa havikidhi vigezo.

“Tutakwenda kumalizia mchakato wa mabadiliko ili kila mwanachama aweze kumiliki hisa zake, suala la tano ni miundo mbinu yetu ya eneo la viwanja nayo tutaiboresha ili iendane na hadhi ya Simba.

MO Dewji amemalizia kwa kutaja eneo la uwekezaji kwa soka la vijana na kwamba wataweka nguvu kubwa itakayozalisha vipaji kwa kuanzia chini.

Huku akisema kuwa ameongea na Try Again na amekubali kubaki kama mjumbe wa bodi upande wa mwekezaji. Meridianbet kasino ya mtandaoni ni mgodi wa ushindi na utajiri.

Acha ujumbe