Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Simba SC, Salim Abdallah Try Again ametangaza kuachia nafasi yake, n kumuomba Muwekezaji wa timu hiyo Mohammed Dewji kuchukua nafasi yake. Jisajili Meridianbet uwe tajiri na milionea.
Salim Try Again amefikia uamuzi huo baada ya yanayoendelea katika klabu hiyo kwa siku za hivi karibuni, hivyo kutoka na kuiongoza Simba kwa miaka 7 sasa ni wakati wake wa kuachia wengine.
“Nimemuomba Mohammed Dewji aje kuwa Mwenyekiti wa Bodi kama atakubali, nimekubali na kwa maana hiyo sasa natoka kuwa mwenyekiti wa Bodi, nitabaki kuwa kama mwanachama wa kawaida wa Simba na Mpenzi, na nitaitumikia Simba kwa namna yeyote”
“Mimi ni mdogo kuliko klabu, nimekaa miaka 7 lakini sasa nimeona niachie ngazi hii, niwashukuru viongozi wengine na bodi, hawa waliobaki tuwape sapoti, tuondoe migogoro tuwe nguvu moja, tumpe sapoti Mohammed Dewji” Alisema Salim Abdallah.
Pia aligusia suala la wachezaji wa timu hiyo kuihujumu Simba kwenye mechi zake, na kama Uongozi wameligundua hilo na umeanza kulifanyia kazi jambo hilo, ikiwemo kuwaacha baadhi ya wachezaji. Ligi zinakaribia kurudi, Bashiri na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo 1000+
“Simba akicheza na kimataifa anacheza mpira mzuri, lakini akicheza na Ihefu hawachezi, ni usaliti tumegundua, viongozi tunalifanyia kazi mchezo huu mchafu na hukubaliki kwa klabu yatu”