Douglas Luiz Anukia Juventus

Kiungo wa kimataifa wa Brazil anayekipiga kwenye klabu ya Aston Villa ya nchini Uingereza Dougals Luiz inaelezwa yuko mbioni kujiunga na klabu ya Juventus ya nchini Italia kuelekea msimu ujao.

Douglas Luiz mwenye umri wa miaka (26) amekua akifuatiliwa kwa karibu na klabu ya Juventus na mpaka sasa vigogo hao wa soka nchini Italia wamefikia hatua nzuri ya kumchukua kiungo huyo, Kwani mchezaji huyo ameshakubaliana na klabu hiyo na kilichobaki ni klabu yake ya Aston Villa kuidhinidha usajili huo.

Masharti ambayo klabu ya Aston Villa wameyatoa kwa klabu ya Juventus ili kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil kujiunga nao ni pamoja kupata mchezaji mmoja kutoka klabu hiyo nchini Italia ajiunge na Aston Villa, Mpaka sasa inaelezwa mchezaji raia wa Marekani Winston Mckienne ndio amejumuishwa kwenye dili hilo.

Klabu ya Juventus wapo kwenye mkakati mzito wa kuiboresha timu hiyo ili kuirejesha kwenye makali yake ambayo imekua nayo miaka kadhaa nyuma, Hivo njia mojawapo ni kuhakikisha wanaingia sokoni na kusajili wachezaji wenye ubora mkubwa lakini pia kuwaongezea mikataba wachezaji wao muhimu klabuni kama wanavyofanya kwasasa.

Kiungo Douglas Luiz ameivutia klabu ya Juventus kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha ndani ya klabu ya Aston Villa kwa misimu miwili mfululizo sasa, Jambo ambalo linaaminika hata wasingejitokeza Juventus basi klabu nyingine kubwa ingeulizia huduma yake kwani amekua moja ya wachezaji muhimu na bora sana ndani ya klabu ya Aston Villa yenye maskani yake Villa Park.

Acha ujumbe