Kiungo wa kimataifa wa Italia anayekipiga ndani ya klabu ya Inter Milan Nicolo Barella anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa ligi kuu nchini Italia Serie A.
Klabu ya Inter Milan imekua ikifanya mazungumzo na wachezaji wake muhimu klabuni hapo kwajili ya kuwaongezea mikataba ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo, Huku mmoja wao akiwa ni kiungo Nicolo Barella ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa mafanikio ndani ya miaka kadhaa.Mabingwa hao wa soka nchini Italia wana mpango wa kuendelea kutawala soka la Italia baada ya kufanikiwa kutwaa taji la ligi kuu msimu huu, Huku ikiwa ndio sababu kubwa ya kutaka kuwabakiza wachezaji bora klabuni hapo lakini pia kuingia sokoni kuwinda wachezaji wenye ubora kuelekea msimu ujao.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Italia inazungumzwa ndio atakua mchezaji wa kwanza kusaini mkataba mpya klabuni hapo, Huku akiwa amejifunga kwelikweli kwani inaelezwa ameongeza mkataba wa miaka mitano ambao utamuweka ndani ya timu hiyo mpaka mwaka 2029.Baada ya Barella kusaini mkataba mpya ndani ya klabu ya Inter Milan mchezaji atakayefuata kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ni nahodha Lautaro Martinez mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina, Lakini pia inaelezwa kocha Simeone Inzaghi amekubali dili la kusalia klabuni hapo na ataongeza mkataba wa miaka mitatu.