Benjamin Sesko Kuongeza Miaka Mitano Rb Leipzig

Mshambuliaji wa klabu ya Rb Leipzig raia wa kimataifa wa Slovenia Benjamin Sesko inaelezwa amekubali dili la mkataba mpya ndani ya klabu hiyo na atasaini mkataba wa miaka mitano ambao utamuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2029.

Benjamin Sesko mwenye umri wa miaka (21) amekua akionesha ubora mkubwa ndani ya klabu ya Rb Leipzig jambo ambalo limekua likivutia vilabu vingi barani ulaya, Lakini mshambuliaji huyo kijana ameamua kuendelea kubaki ndani ya klabu hiyo kutoka nchini Ujerumani mpaka mwaka 2029.benjamin seskoMshambuliaji huyo wa kimataifa wa Slovenia amekua akifuatiliwa na vilabu kadhaa ambapo klabu ambayo ilikua ikimfuatilia zaidi siku za hivi karibuni ni klabu ya Arsenal, Hivo mchezaji huyo kuongeza mkataba mpya ndani ya Rb Leipzig sio habari nzuri kwa washika mitutu hao kutoka jiji la London.

Taarifa zinaeleza mchezaji huyo anatarajiwa kusaini mkataba huo kesho Jumatano huku kukiwa na kipengele ambacho kitamruhu mchezaji huyo kutimka klabuni hapo mwaka 2025 au 2026, Huku mkataba mpya ukimfanya yeye kama taswira ya mradi mpya klabuni hapo.benjamin seskoKlabu ya Rb Leipzig imekua ikisifika kwa kutoa wachezaji wenye ubora mkubwa miaka ya hivi karibuni na hii inatokana na ubora wao kutafuta vipaji barani ulaya na nje ya bara la ulaya, Jambo ambalo limefanya kupata vipaji vingi kama vya mshambuliaji Benjamin Sesko ambaye atasaini mkataba wake mpya kesho ndani ya timu hiyo.

Acha ujumbe