Manchester City Wamuongezea Ortega Mkataba

Klabu ya Manchester City imemuongezea mkataba golikipa wake namba mbili Stefan Ortega mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo mpaka mwaka 2026.

Ortega amekua na msimu mzuri ndani ya klabu ya Manchester City kwani pale ambapo golikipa namba moja Ederson Moraes amekua akikosekana yeye alionesha kiwango kikubwa kilichowavutia Man City kumuongezea mkataba.manchester cityGolikipa huyo raia wa kimataifa wa Ujerumani ataendelea kuwepo kwenye viunga vya Etihad mpaka mwaka 2026, Hii ikiwa imekuja kutokana na ambacho amekionesha msimu uliomalizika.

Ederson Moraes ambaye ni golikipa namba moja wa klabu ya Manchester City inaelezwa anaweza kutimka klabuni hapo na kuelekea nchini Saudia Arabia, Hivo mabingwa hao wa Uingereza wakaamua kumuongezea mkataba Ortega.manchester cityManchester City licha ya kumuongezea mkataba wa miaka miwili Ortega lakini mapenzi yao ni kutaka kumbakiza golikipa Ederson Moraes ndani ya timu, Kwani mpaka sasa mazungumzo yanaendelea baina ya pande zote mbili.

 

Acha ujumbe