LICHA ya kubaki siku nane kabla ya Yanga kuvaana na Al Merrikh ya Sudan kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, tayari Yanga wameshakuwa gumzo nchini Rwanda ambapo utapigwa mchezo huo huku baadhi ya nyota wake wakiwa wameiteka nchi hiyo kwa kutajwa sana na mashabiki.

Miongoni mwa majina ambayo yanazungumzwa zaidi kwa mastaa wa Yanga ni kiungo mshambuliaji Maxi Mpia Nzengeli na Pacome Zouzoua ambao licha ya kusajiliwa msimu huu wamekuwa moto kutokana na uwezo waliounyesha klabuni hapo.YANGAChanzo kutoka nchini Rwanda kimeliambia Championi Ijumaa, kuwa nyota hao wawili sambamba na wengine wa timu hiyo wamekuwa wakitajwa kwa wingi na mashabiki wamejiandaa vilivyo kuwatazama siku ya mechi hiyo.

“Unajua tangu msimu unaanza mashabiki wamekuwa hapa nchini wamekuwa wakiifuatilia Yanga kwa ukaribu na viwango vya mastaa wa timu hiyo wamekuwa wakivijua, ndiyo maana wanawazungumzia sana.YANGA“Nadhani siku ya mechi hiyo kutakuwa na idadi kubwa ya mashabiki ambao watajitokeza uwanjani kwa kuwa watataka kuwaona wenyewe namna wanavyocheza na viwango vyao kama wanavyowaona sasa kwenye runinga,” kilisema chanzo hicho.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa