MGUNDA: CHAMA SIO MKUBWA KULIKO SIMBA

KOCHA wa Simba Juma Mgunda amesema kuwa, wao kama klabu wameshasahau kuhusiana na Clatous Chama Kwa kuwa wao ni timu na ni taasisi kubwa.

 

Mgunda alisema hakuna mchezaji mkubwa kuliko klabu na wao kama Simba akili zao zimeegemea kwenye kutengeneza timu mpya.Mgunda

Mgunda aliiambia Meridian Sports kuwa Kama Chama aliamua kuondoka ilikuwa ni Kwa uamuzi wake mwenyewe na hawakuwa na Sababu ya kung’ang’ania kuwa naye Kwa kuwa alishafanya maamuzi.

 

“Timu ni kubwa kuliko mchezaji, huyo Chama anayeimbwa sana, alishamaliza mkataba na akaamua kutafuta changamoto nyingine. Kwahiyo sisi tunapambana kutengeneza timu mpya na hayo ya Chama yameshapita,” alisema.

Acha ujumbe