Mkude kila kitu fresh Bukoba

KIUNGO na Mchezaji wa muda mrefu ndani ya Simba Jonas Mkude ni miongoni mwa nyota wa kikosi cha Simba ambao wapo kwenye msafara ulioweka kambi Bukoba.

Kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda kina kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.

Ikumbukwe kwamba Simba msimu wa 2021/22 ilinyooshwa bao 1-0 na Kagera Sugar katika mchezo uliochezwa Kaitaba kwa bao la Kiiza Diego ambaye alifunga akitokea benchi.

Mkude kila kitu fresh Bukoba

Pia alionyeshwa kadi mbili za njano zilizofanya akaonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo huo ambao Simba walianza kupoteza dira ya kutetea ubingwa wao ambao ulisepa na Yanga.

Mkude kila kitu fresh Bukoba

Mbali na Mkude viungo Clatous Chama, Pape Sakho, Jonas Mkude, Erasto Nyoni nao ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye kikosi hicho

Mchezaji huyo pia amekuwa hana wakati mzuri kwa sasa ndani ya Simba na amekosekana kwenye baadhi ya mechi za timu hiyo na kuzua hofu kuhusu mustakabali wake.

Acha ujumbe